#
.

Tuesday, February 5, 2013

Mhe.Mohammed Razza ni muwakilishi wa Jimbo la Uzini ambaye amechukua nafasi hiyo baada ya kifo cha Mhe.Mussa Khamisi Silima katika kura za Matawi. Alimpiku mpizani wake Ndg.Tafana Kassim Mzee kwa kura 1,963 katika matawi 16 na Ndg.Tafana Kassim Mzee alipata kura 79 katika Matawi 16 na kuwapiku wengi.Katika uchaguzi uliofanyika ulioshirikisha vyama vya Upizani kama Chadema,Cuf na vyengine. Alifanikiwa kuwa kinara katika Jimbo hilo, hii ilitoa taswira mpya kwa wakazi wa Jimbo la hilo. Sasa kuna maswali mengi ungependa kujiuliza, je ahadi alizotoa je baadhi amefanikiwa? Je kweli anafaa kuwa muwakilishi wa jibo hilo? Ukweli Mhe. Mohammed Raza amefanikiwa kwa kiasi kikubwa mfano katika kutimiza miaka yake Hamsini ya kuzaliwa siku ambayo Wazanzibari wote na Watanzania bara hawatoisahau siku iliyo zama boti ya abiria ya Mv.Skygati ( Saidi Mbuzi).Alifanikiwa kujenga madarasa mawili yenye hazi nzuri katika shule ya msingi ya Pagali pamoja na barabara yake pia kuweka mataa katika kiwanja cha michezo cha uzini na kuzungushia waya uwanja mzima pamoja na kutoa vifaa vya michezo kwa timu zisizo pungua 21.Haya ni baadhi ya machache tu aliyo fanya ila kuna mengi ameyafanya zaidi ya haya.